Eriksen Kurejea Msimu huu

Kiungo wa klabu ya Manchester United Christian Eriksen kurejea tena klabuni hapo ndani ya msimu huu baada ya kupata majeraha kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag.

Christian Eriksen ambaye alipata mapema mwezi Januari baada ya kuumia enka yake katika mchezo wa kombe la Fa dhidi ya klabu ya Reading na kumfanya kukaa nje kuanzia mwezi huo mpaka sasa, Lakini kocha Ten Hag amesema kiungo huyo ataitumikia klabu hiyo tena msimu huu kabla haujamalizika.eriksenKiungo huyo wa kimataifa wa Denmark alifanikiwa kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi hicho akitengeneza safu bora ya kiungo akiwa na wachezaji wenzake kama Casemiro pamoja na Bruno Fernandes, Hivo kuumia kwake kuliacha pengo ndani ya klabu hiyo.

Kocha Ten Hag amesema hawezi kusema ni lini kiungo huyo atarejea ndani ya timu hiyo lakini anachojua kwasasa Eriksen anaendelea vizuri, Hivo atarejea kabla ya msimu huu kumalizika na kuanza kuitumikia klabu hiyo baada ya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.eriksenKlabu ya Manchester United imekubwa na wachezaji wawili ambao wamepata majeraha ya muda mrefu msimu huu akiwemo Christian Eriksen, Lakini kiungo mwingine Donny Van de Beek yeye hataweza kurejea tena uwanjani baada ya kuumia goti lake na kufanyiwa upasuaji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.