Sampaoli Akalia Kuti Kavu Sevilla

Aliyekua kocha wa klabu ya Sevilla George Sampaoli ametimuliwa ndani ya klabu hiyo baada ya mabosi wa klabu hiyo kutoridhishwa na mwenendo wa kocha huyo ndani ya timu hiyo.

Kocha huyo Sampaoli amekua kwenye wakati mgumu ndani ya timu hiyo kutoka na mfululizo wa matokeo mabaya ndani ya timu hiyo, Hivo waajiri wake kufikia uamuzi wa kumtimua kocha huyo ndani ya klabu ya Sevilla mpaka sasa wapo kwenye wakati mgumu kwenye ligi kuu nchini Hispania.sampaoliKlabu ya Sevilla imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Europa League lakini ikiwa kwenye wakati mgumu zaidi kwenye ligi ya nyumbani nchini humo maarufu kama La liga, Kwani klabu ya Sevilla inakamata nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kocha Sampaoli amejiunga na klabu ya Sevilla msimu huu baada ya kuondoka kwa alieyekua kocha wa klabu hiyo Julien Lopetegui kutimkia nchini Uingereza kujiunga na klabu ya Woves, Lakini kutokana na mwenendo wa klabu hiyo siku za karibuni umemfanya kocha huyo kutimuliwa.sampaoliKocha Jose Luis Mendilibar ni kocha ambae atakuchukua mikoba ya kocha wa klabu ya Sevilla aliyetimuliwa George Sampaoli, Kocha Mendilibar ataifundisha klabu hiyo mpaka mwezi Juni mwaka huu ikiwa ni mpaka mwisho wa msimu ndipo klabu hiyo iamue kama itampa mkataba wa kudumu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.