Jorge Sampaoli kocha wa klabu ya Sevilla amesema klabu hiyo itatoa tamko kuhusu nyota wake Isco ambaye inataarifiwa yuko mbioni kuvunja mkataba na timu hiyo.

Kocha huyo amesema mpaka sasa yeye hajahusishwa kwenye lolote kuhusu mchezaji Isco na hata suala la mchezaji kutaka kuvunja mkataba na klabu hiyo yeye kwake hana na taarifa nalo, Hivo kuwataka watu kutulia na klabu hiyo itakuja na tamkorasmi juu ya suala hilo.sampaoliMchezaji Isco amejiunga klabuni hapo mwezi Agosti mwaka huu akitokea klabu ya Real Madrid ambapo aliishi kwa takribani miaka kumi, Huku alijiunga na klabu ya Sevilla lakini kuna taarifa zinasema mchezaji huyo yuko mbioni kuvunja mkataba na klabu hiyo.

Isco amekua mchezaji muhimu tangu ajiunge klabuni hapo kwani amefanikiwa kucheza michezo 19 huku akifanikiwa kuanza michezo 16, Pia amefanikiwa kuhusika kwenye mabao manne akifunga moja na kupiga pasi tatu za mabao.sampaoliKlabu mbalimbali zinahusishwa kuhitaji saini ya Isco baada ya taarifa hizi kusambaa na miongoni mwa vilabu hivo ni pamoja na Napoli, Juventus, Aston Villa pamoja kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid kwasasa akiwa Wolves Julien Lopetegui inaelezwa anahitaji huduma ya kiungo huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa