Shirikisho la soka nchini Ufaransa (FFF) limelaani vikali kitendo cha wachezaji wa timu ya ya taifa wenye asili ya Afrika kubaguliwa baada ya kufungwa kwenye fainali ya kombe la dunia wikiendi iliyopita.
Baada ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia kati ya Ufaransa na Argentina kuna wachezaji takribani watatu wenye asili ya Afrika walikumbana na ubaguzi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Wachezaji ni kiungo Aurelien Tchouameni aliokosa mkwaju wa penati, Kolo Muani, Pamoja na Kingsley Coman nae akikosa penati katika mchezo huo.Kufuatia kitendo hicho shirikisho la soka nchini humo linalojulikana kama (FFF) limelaani kitendo hicho baada ya kuposti na kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter na kuandika “Baada ya fainali za kombe la dunia, Wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa walikubwa na matamshi ya kibaguzi na yasiyokubalika na ya chuki kwenye mitandao ya kijamii. FFF inawalaani na itawasilisha malalamiko dhidi ya waliohusika”
Shirikisho hilo limeonesha kukerwa kwa kitendo kilichooneshwa na mashabiki wa nchi hiyo, Kwani kitendo ambacho wamefanya mashabiki wa timu ya taifa ya Ufaransa sio cha kiungwana wala cha kiunamichezo.Hii imekua kawaida sasa kwa wachezaji wenye asili ya Afrikawanaocheza timu za taifa za ulaya kubaguliwa pale wanapokosea au kuteleza kwenye jambo fulani, Kwani mwaka 2021 kwenye michuano ya Euro mchezo wa fainali kati ya Uingereza dhidi ya Italia ambapo wachezaji Marcus Rashford, Jadon Sancho, na Bukayo Saka walifanyiwa vitendo vya kibaguzi baada ya kukosa penati kwenye mchezo huo.