Kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa inaandamwa na ugonjwa ambao bado haujafahamika ambapo wimbi la wachezaji wa timu hiyo wanaendelea kuumwa na kuongezeka.
Timu hiyo ambayo imebakiza siku moja kuelekea kucheza mchezo wake wa fainali siku ya jumapili dhidi ya timu ya taifa ya Argentina, Ambapo mabingwa hao watetezi watakua wanacheza fainali yao ya pili mfululizo.Timu ya taifa ya Ufaransa iliwakosa wachezaji wake wawili katika mchezo wa nusu fainali siku ya jumatano dhidi ya Morocco ambao ni Adrien Rabiot na beki Dayot Upamecano kutokana na kuumwa siku kadhaa kabla ya mchezo.
Taarifa zimeleza kua beki tegemezi wa timu hiyo Raphael Varane, na Ibrahim Konate hawajafanya mazoezi na timu siku ya leo, Hii inaleta taharuki kwenye kikosi cha Deschamps kinachotarajia kwenda kutetea taji lake.Timu ya Ufaransa taifa imepokea taarifa za matumaini baada ya wachezaji wake wawili waliokua kwenye ugonjwa Rabiot na Upamecano kuelezwa kurejesha utimamu wao na wako tayari kwa mtanange wa fainali siku ya jumapili.