Mchezaji wa Timu ya KMC FC Matheo Antony ambaye jana alishindwa kuendelea na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania bara dhidi ya Coastal Union ya mkoani Tanga baada ya kupata majeraha anaendelea na matibabu na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Matheo ambaye anaongoza kwa magoli Manne katika kikosi hicho cha KMC FC alipata majeraha jana baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wa Coastal Union na hivyo kupelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu hali iliyolazimika kushonwa nyuzi Nne.KMC” Mchezaji wetu Matheo jana aliumia baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wa Coastal Union hali ambayo ilipelekea kushindwa kuendelea na mchezo na hivyo kukimbizwa Hospitali na garia wagonjwa, lakini alipata matibabu na hivyo anaendelea vizuri , tuzidi kumuombea kwa mwenyezi Mungu apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake.

Aidha katika hatua nyingine , Timu ya KMC FC baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila jana dhidi ya Coastal Union kesho kitaendelea tena na maandalizi kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Alhamisi ya Disemba 22 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.KMCTimu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana jana ilianza vema mzunguko wa pili kwa kuwapiga Coastal Union na hivyo kukusanya alama zote tatu muhimu goli lililofungwa na George Makang’a.

” Tunamshukuru Mungu jana tumeanza vema mzunguko wa pili na sasa tunaendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo unaokuja, tunafahamu kabisa mzunguko huu hautakuwa mwepesi hivyo hatuna mashaka kikubwa tutaendela kujiweka imara ili kufanya vizuri kwa kila mchezo.

Tumewapa mapumziko ya siku moja wachezaji wetu ili kuwa na hari na morali zaidi kwenye mchezo unaokuja, tunafahamu kuwa tunamchezo mwingine mgumu lakini kwakuwa tunakikosi bora na chenye ushindani tutaendelea kujiweka imara huku tukiwaheshimu wa pinzani wetu.

Hata hivyo KMC FC baada ya ushindi wa mchezo wa jana, imepanda nafasi moja kutoka nafasi ya 10 mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC hadi nafasi ya tisa huku ikikusanya jumla ya alama 19.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa