Dalic Atamani Modric Awepo Euro 2024

Kocha wa timu ya taifa ya Croatia Zlatko Dalic anatamani kuona nahodha wake Luca Modric anakuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Croatia mpaka kwenye michuano ya Euro 2024.

Kiungo Luca Modric amekua na michuano mizuri sana na kufanikiwa kuifikisha timu yake hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, Licha ya umri wake wa miaka 37 lakini Modric amekua akionesha ubora mkubwa sana.dalicBaada ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la dunia siku ya jumanne dhidi ya Argentina kiungo huyo aligoma kuongea chochote kuhusu hatma yake na timu ya taifa ya Croatia, Hivo mpaka wakati haijajulikana kama ataendelea kuwepo au hatakuepo.

Kocha Dalic anasema anaamini mchezaji huyo atakuepo mpaka miezi 18 ijayo ikiwa ni muda wa mwaka mmoja na miezi sita ambapo michuano ya Euro 2024 ndipo itakua inapigwa nchini Ujerumani.dalicTimu ya taifa ya Croatia chini ya kocha Zlatko Dalic itakwenda kucheza mchezo wa mshindi wa tatu wa kombe la dunia siku ya kesho dhidi ya timu ya taifa Morocco, Mchezo utakaopigwa katika dimba la Khalifa International.

Acha ujumbe