Giroud: Ufaransa Ilionyesha "Mentality ya 2018" Kuifunga Uingereza

Olivier Giroud amelinganisha ushindi mnono wa Ufaransa katika robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Uingereza hapo jana na ushindi wao wa nusu fainali dhidi ya Ubelgiji miaka minne iliyopita.

 

Giroud: Ufaransa Ilionyesha "Mentality ya 2018" Kuifunga Uingereza

Ufaransa ilicharaza Uingereza mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Al Bayt hapo jana, huku Giroud akipachika bao wavuni kwa mpira wa kichwani dakika ya 78 na kufanya ubao kusomeka tofauti.

Aurelien Tchouameni alikuwa amewatanguliza mabingwa hao watetezi wa Dunia mbele, lakini Uingereza ilijibu vikali na kusawazisha kupitia kwa Harry Kane kwa mkwaju wa penalti.

Kikosi cha Gareth Southgate kilikuwa na uwezo wa kusawazisha bao hilo kwani walipata mkwaju wa penalti lakini wakshindwa kuutumia baada ya Harry Kane kupaisha mkwaju huo wa penalti juu ya lango.

Giroud: Ufaransa Ilionyesha "Mentality ya 2018" Kuifunga Uingereza

Ushindi huo unaipeleka Ufaransa katika nusu fainali dhidi ya Morocco, huku timu ya Didier Deschamps ikionekana kuwa bora zaidi kutetea taji lao, lakini droo hiyo ilionyesha kuwa ngumu kushinda Kombe la Dunia, huku Giroud akikumbushwa kichapo cha moja kwa bila kutoka kwa Ubelgiji nchini Urusi.

Giroud amesema kuwa;“Mechi ya leo usiku ilikumbusha mechi dhidi ya Ubelgiji 2018, tulipigana jino na kucha. Walirudi kwenye mechi, walianza kuamini lakini tulionyesha tunaweza kuwa hatari kwenye shambulio la kaunta.”

Hakuishia hapo bali aliendelea kwa kusema kuwa walikuwa na bahati kidogo kwasababu Kane alikosa penalti, lakini walijitolea na kupigana jino na kucha na inamkumbusha mawazo ya 2018, na kundi lao linastahili kufika huko.

Giroud: Ufaransa Ilionyesha "Mentality ya 2018" Kuifunga Uingereza

Giroud alisawazisha na kisha kupita rekodi ya Thierry Henry ya Ufaransa ya mabao 53 mapema katika fainali hizo, na anasema kuwa mabao yote ni muhimu ukweli ni kwamba alimtangulia Thierry Henry na nafasi ya 52, lakini hii ya 53 labda ni bora zaidi.

“Dakika moja kabla, nilikuwa na nafasi na ningeweza kufunga. Nilidhani ningepata nafasi nyingine, na haikuaminika kufunga.”

Acha ujumbe