Mshambuliaji wa klabu ya Napoli raia wa Nigeria Victor Osimhen amesema kwasasa yeye anawaza kuipatia klabu yake ya Napoli taji la ligi kuu maarufu kama Scudetto na tetesi za usajili hazina nafasi kwasasa kwake.

Mshambuliaji huyo ambaye anaongoza mbio za ufungfaji baada ya kufunga mabao tisa na kuisaidia klabu yake ya Napoli kukaa kileleni kwa alama nane kabla mapumziko ya michuano ya kombe la dunia.osimhenKlabu ya Napoli ambayo inaongoza ligi kuu ya Italia mpaka kufikia mapumziko ya kombe la dunia, Klabu hiyo ya Napoli inahitaji kushinda ubingwa wa ligi hiyo sana kwasababu klabu hiyo imekua ikiutafuta ubingwa huo kwa muda mrefu kwani mara ya mwisho ilikua msimu wa 1989/90.

Mshambuliaji Victor Osimhen amesema kwasasa hakuna kikubwa zaidi ya kushinda taji la ligi kuu ya Italia, Mshambuliaji huyo anaeleza kua ni ngumu kufikiria kitu bora zaidi ya Napoli kwasasa hivo nyota huyo anaeleza kua mipango ni kubeba ubingwa wa Scudetto.osimhenMshambuliaji Victor Osimhen amekua akifuatiliwa na vilabu tofauti tofauti kutokana ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu ya Napoli, Moja ya vilabu ambavyo vinamfatilia mshambuliaji huyo ni klabu ya Manchester United.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa