Alonso Kwenye Rada za Real Madrid

Kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen Xabi Alonso ameingia kwenye rada za klabu ya Real Madrid na kutajwa kama mrithi wa kocha wasasa wa klabu hiyo kocha Carlo Ancelotti ambaye anatajwa kuondolewa klabuni hapo.

Xabi Alonso amekua kwenye kiwango kizuri ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen tangu aichukue timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu, Hivo kutokana na hali imemvutia rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez na kutaka kumrejesha ndani ya klabu hiyo msimu unaofuata.alonsoReal Madrid inasemekana inataka kuachana na kocha Carlo Ancelotti mwishoni mwa msimu huu kutokana na matokeo ya kusuasua yanayoendelea ndani ya klabu hiyo, Huku mpaka sasa wakionekana kulipoteza taji la ligi kuu nchini humo baada ya kuachwa kwa alama 12 dhidi ya wapinzani wao klabu ya Barcelona.

Xabi Alonso ameiongoza klabu ya Bayern Leverkusen kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Uefa Europa League, Huku kwenye ligi kuu ya Ujerumani wakiwa hawapo vibaya sana kwani mpaka sasa wanakamata nafasi ya nane kwenye ligi kuu ya Ujerumani huku kukiwa na uwezekano wa kupanda zaidi.alonsoGwiji Alonso ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Real Madrid amefanikiwa kuibadilisha klabu ya Leverkusen kwa kiwango kikubwa, Huku akitajwa kua moja ya makocha bora vijana wanaokuja kwa kasi katika ulimwengu wa soka hivo ni wazi akiendelea na ubora huo anawez kupewa jukumu la kuvaa viatu vya Carlo Ancelotti.

Acha ujumbe