Tchouameni Hajakata Tamaa

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Aurelien Tchouameni amekua akipitia kipindi kigumu kwenye klabu ya Real Madrid lakini inaelezwa hajakata tamaa na ataendelea kupambana zaidi.

Tchouameni anaonekana kupoteza nafasi ndani ya kikosi cha Real Madrid baada ya kupata majeraha mapema baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia, Taarifa zinaeleza mchezaji huyo anachukulia hali hiyo kama sehemu ya mapito lakini anaweza kurudi na kuanza kufanya vizuri.TchouameniKiungo huyo ambaye amejiunga na klabu ya Real Madrid kwenye dirisha kubwa lililopita akitokea Monaco, Huku kukiwa na matarajio makubwa kutoka kwake kuchukua nafasi ya Carlos Casemiro aliyetimkia klabu ya Manchester United lakini kwasasa anaonekana kupoteza nafasi.

Eduardo Camavinga ambaye ni raia wa kimataifa wa Ufaransa anaonekana kuchukua nafasi ya kiungo mwenzake Tchouameni kwenye kikosi cha Real Madrid, Lakini Aurelien amejikita kwenye kujituma zaidi ili kuweza kurudisha nafasi yake kwenye kikosi cha Carlo Ancelotti.TchouameniAurelien Tchouameni hawazi suala la kukata tamaa wala kutupa taulo ulingoni kama ambavyo imekua kwa wachezaji wengine wanapopoteza nafasi kwenye timu, Lakini mchezaji huyo anaamini hatawaangusha mashabiki wa klabu hiyo kwani atarudi kwa nguvu na kuanza kufanya vizuri na kufurahisha mashabiki wake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.