Rooney Kuifundisha MLS All-Star

Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney anatarajwa kuifundisha timu ya mastaa wanaocheza ligi kuu nchini Marekani katika mchezo dhidi ya klabu ya Arsenal unaotarajiwa kupigwa mwezi Julai.

Wayne Rooney amekua akifundisha klabu ya DC United ya nchini Marekani baada ya kuondoka klabu ya Derby County, Hivo ni kocha ambae amekua kwenye ubora mzuri ndani ya Marekani hivo hiyo imepelekea kushawishi kupewa timu ya mastaa wa ligi kuu ya Marekani.RooneyKwa miaka miwili timu ya mastaa wa Marekani imekua ikicheza dhidi ya kikosi cha mastaa wa La liga, Lakini msimu inatarajiwa kucheza tena na timu kutoka ligi kuu ya Uingereza na timu hiyo itakua klabu ya Arsenal ambayo ndio itakipiga na timu ya mastaa wa ligi kuu nchini Marekani.

Wayne Rooney ameonesha kufurahishwa na kitendo cha kupewa timu ya mastaa ya ligi kuu nchini Marekani, Kwani anaeleza amekua siti ya mbele kabisa akishuhudia ukuaji wa ligi kuu nchini Marekani kama mchezaji na kama kocha na kueleza kwake ni litakua jambo lisilosahaulika sana.RooneyMbali na Rooney ambaye atakiongoza kikosi cha mastaa wa ligi kuu nchini Marekani lakini kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amesema ziara yao ya nchini Marekani mwaka huu litakua jambo zuri kwao, Kwani watakwenda kucheza dhidi ya mastaa wa ligi kuu ya Marekani.

Acha ujumbe