Ibrahimovic Alihitaji Operesheni Tatu ili Aendelee Kucheza Mpira

Mshambuliaji wa klabu ya Ac Milan Zlatan Ibrahimovic amesema alihitaji kufanyiwa operesheni tatu za goti msimu uliomalizika ili kuweza kuokoa maisha yake ya soka na mpaka sasa anaendelea kucheza soka.

Zlatan Ibrahimovic amekua akisumbuliwa na majeraha kwa mda mrefu hasa msimu uliomalizika na kumfanya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, Lakini ameweka wazi kua ilihitajika operesheni tatu za goti ili aweze kuendelea kucheza mpira.IbrahimovicMshambuliaji huyo ameyazungumza hayo katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2024, Timu ya taifa ya Sweden itakipiga na timu ya taifa ya Ubelgiji mapema wiki hii kuelekea kufuzu Euro mwakani.

Ibrahimovic ameweka wazi operesheni alizofanya zilimpa wakati mgumu sana kwakua kila alipokua anapiga hatua mbele, Lakini anarudi hatua mbili nyuma jambo ambalo lilikua likimpa wakati mgumu sana, Lakini hatimae mwishoni alikuja kupata mwanga na kupona na mpaka sasa anacheza mpira.IbrahimovicMshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Sweden baada ya muda mrefu kupita, Lakini kocha wasasa wa timu ya taifa ya nchini hiyo Janne Andersson amemuita staa huyo ambaye alishawahi kutangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo ya taifa miaka kadhaa nyuma kabla ya kutangaza kurejea tena.

Acha ujumbe