Sakata la mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum ambaye aliomba kuondoka ndani ya klabu hiyo limepigwa tarehe tena na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kupitia shirikisho la mpira Tanzania TFF mpaka tarehe 4 mwezi Mei.
Mchezaji Feisal Salum ambaye amekua kwenye msuguano na klabu yake ya Yanga tangu mwishoni mwa mwaka jana na kesi kufunguliwa na klabu yake baada ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kinyume na sheria kama walivyoeleza Yanga kwenye shauri lao leo kamati imeweza kusogeza mbele tena shauri hilo.
Shauri la mchezaji huyo lilipangwa kusikilizwa leo ikiwa ni baada ya kamati hiyo kutoa maamuzi kua mchezaji huyo ni mali ya klabu ya Yanga, Lakini jopo la mawakili kwa kusahirikiana na mchezaji lilikata rufaa kupinga madai hayo jambo ambalo limeendelea kufanya shauri hilo kuwepo ndani ya TFF.
Feisal leo alionekana akiwa na mawakili wake katika makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF kwajili ya kusikiliza shauri lake ambalo ameomba shirikisho la soka kuweza kuingilia kati shauri hilo na kuvunja mkataba wake na klabu hiyo kwa kile alichokieleza kua hakua na anapata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo na kupitia manyanyaso vilevile ndani ya timu hiyo.
Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji chini ya mwamvuli wa TFF itakutana tena tarehe 4 mwezi Mei ili kuweza kusikiliza shauri hilo kutoka kwa mchezaji Feisal Salum ambaye ni wazi hataki kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga tena, Huku mpaka sasa yeye na jopo lake wakiwa wameshindwa shauri hilo mara mbili na klabu yake ya Yanga.

