Bayern Munich Yalaani Ubaguzi kwa Upamecano

Klabu ya Fc Bayern Munich imeripotiwa kulaani kitendo cha beki wake raia wa kimataifa wa Ufaransa Dayot Upamecano kufanyiwa vitendo vya kibaguzi baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Manchester City.

Dayot Upamecano alikutana na kadhia ya ubaguzi baada ya kufanya kosa katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Man City kosa ambalo lilipelekea bao la pili, Hivo baada ya kosa hilo ilipelekea mashabiki wa klabu ya Bayern Munich kuanza kumshambulia na maneno ya kibaguzi.Bayern MunichKupitia chapisho la klabu ya Bayern Munich katika mtandao wao wa kijamii pale Instagram wameandika “Sisi sote kutoka Bayern tunalaani ubaguzi wa rangi kwa maneno makali iwezekanavyo, Klabu ipo nyuma yako Upamecano” Kupitia andiko hilo klabu hiyo imeonesha ipo nyuma ya beki huyo na kupinga ubaguzi huo.

Kumekua na mwendelezo wa mashabiki wa klabu mbalimbali kufanya vitendo vya ubaguzi kwa wachezaji wa timu zao pale ambapo inatokea wanafanya makosa uwanjani, Lakini shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA lilitangaza kuhakikisha itadhdbiti ubaguzi wa rangi baada ya michuano ya kombe la dunia Qatar.Bayern MunichKlabu ya Bayern Munich ilijikuta kwenye wakati mgumu kwenye uwanja wa Etihad usiku wa jana baada ya kujikuta wakiambulia kichapo cha mabao matatu kwa bila dhidi ya klabu ya Manchester City, Hivo kufanya mlima kua mkubwa sana kuelekea mchezo utakaopigwa katika dimba la Allianz Arena.

Acha ujumbe