Klabu ya Fc Bayern Munich imefanikiwa kupata matokeo ya ushhindi katika ligi kuu ya Ujerumani baada ya kuifunga klabu ya Bochum kwa magoli matatu kwa bila wakiwa katika dimba lao la nyumbani la Allianz Arena.
Klabu ya Byern Munich ambayo imefanikiwa kushinda mchezo wake wa pili mfululizo katika ligi kuu ya Ujerumani baada ya kuifunga Wolsburg wikiendi iliyomalizika, na kufanikiwa kuibamiza Bochum kwa mabao matatu kwa bila katika mchezo wa leo.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Ujerumani waliweza kushinda mchezo huo huku wakiutawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa, Magoli ya klabu hiyo yalipatikana kupitia kwa Thomas Muller, Kingsley Coman, pamoja na Serge Gnabry aliepiga msumari wa mwisho.
Klabu ya Bayern Munich ambayo inakwenda kucheza mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya siku ya jumanne dhidi ya klabu ya PSG, Matokeo ya ushindi katika mchezo wa leo yatawafanya kwenda kwenye mchezo huo katika hali nzuri na kujiamini zaidi.
Bayern Munich baada ya kupata matokeo katika mchezo wa leo pia ilishuhudia mshambuliaji wake Thomas Muller akiweka rekodi ya kua mchezaji wa klabu hiyo aliyecheza michezo mingi ya ligi kuu ya Ujerumani akiipiku rekodi ya gwiji wa klabu hiyo Gerd Muller. Thomas Muller amefanikiwa kucheza mchezo wa 428 akivunja rekodi ya Gerd Muller aliyecheza michezo 427.

