Klabu ya soka ya Arsenal imedondosha alama kwa mara nyingine katika mchezo wa pili wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya klabu ya Brentford.
Arsenal wanadondosha alama katika mchezo wa pili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza msimu huu kwa mara ya kwanza, Kwani wikiendi iliyomalizika klabu hiyo ilipoteza mchezo wa ligi hiyo dhidi ya klabu ya Everton na leo kudondosha alama mbili baada ya kulazimishwa sare na Brentford katika uwaja wao wa nyumbani.
Katika mchezo huo vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza walicheza mchezo mzuri huku wakimiliki mchezo vizuri, Lakini pia klabu ya Brentford wakicheza kwa umakini mkubwa zaidi kuhakikisha washika bunduki hao hawapati goli katika mchezo huo.
Klabu ya Arsenal walifanikiwa kupata bao la kuongoza katika mchezo huo kupitia kwa mchezaji alietokea benchi Leandro Trossard mnamo dakika ya 66 ya mchezo kabla ya Brentford kusawazisha kupitia kwa Ivan Toney dakika ya 74 ya mchezo.
Klabu ya Arsenal wanaendelea kua vinara wa ligi kuu ya Uingereza kwa jumla ya alama sita baada ya kufikisha alama 51, Huku klabu ya Manchester City ambao wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 45 na wakifanikiwa kushinda mchezo wao wa kesho dhidi ya Aston Villa wanapunguza pengo la alama mpaka kufikia tatu.

