Tuchel: Anategemea Maajabu Mchezo wa Pili

Kocha wa klabu ya Fc Bayern Munich Thomas Tuchel amesema ana matumaini ya kupindua meza katika mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Manchester City baada ya jana kupoteza kwa mabao matatu kwa bila.

Tuchel anaamini wanaweza kufanya maajabu katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena jumatano ijayo baada ya kupoteza kwa mabao matatu kwa bila jana dhidi ya Manchester City wakiwa katika dimba la Etihad jambo ambalo ni kama limewashangaza Bayern Munich.TuchelKlabu ya Bayern wanahitaji kua kwenye kiwango bora sana katika mchezo wao wa marudiano ambao watawakaribisha klabu ya Manchester City katika uwanja wao wa nyumbani, Kwani vijana wa Pep Guardiola wameonekana kua kwenye ubora mkubwa sana hasa katika mchezo wa jana.

Kocha Tuchel ameanza kuingia kwenye presha baada ya kuchukua kibarua hicho kutoka kwa Julian Nagelsman kwani tayari ameshatolewa kwenye michuano ya kombe la DFB Pokal na mpaka sasa hali ikiwa sio nzuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kutanguliwa kwa mabao matatu.TuchelKocha Thomas Tuchel amesema kua makosa binafsi ndio yalisababisha mpaka kupoteza mchezo dhidi ya City, Lakini hawahitaji kubadilika sana zaidi ni kupambana vizuri ili waweze kufanya vizuri katika mchezo unaoufuata vilevile kocha amesisitiza wanahitaji bahati pia ili kuwafunga Man City.

Acha ujumbe