Arsenal Wadondosha Alama Tena

Klabu ya Arsenal imedondosha alama kwa mara ya pili mfululizo kwenye ligi kuu ya Uingereza hiyo ni baada ya kukubali sare ya mabao mawili kwa mawili leo dhidi ya klabu ya West Ham United katika mchezo wa derby ya London.

Arsenal walifanikiwa kuuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata uongozi wa mabao mawili ya haraka kupitia kwa mshambuliaji wao Gabriel Jesus na nahodha Martin Odegaard, Lakini vijana wa West Ham walifanikiwa kutulia na kuweza kupata bao moja kabla ya mapumziko kupitia kwa Said Benrahma na kufanya mchezo kwenda mapumziko kwa Washika mitutu kua mbele kwa mabao mawili.ArsenalKipindi cha pili Vijana wa Mikel Arteta walionekana kuanza kwa kasi kama ambayo walianza nayo kipindi cha kwanza na kupeleka mashambulizi kwenye lango la West Ham, Mpaka kupekea kupata mkwaju wa penati dakika ya 52 lakini bahati mbaya Bukayo Saka alikosa mkwaju huo.

West Ham walionekana kama wameamka na kupata nguvu baada ya Arsenal kukosa mkwaju wa penati na kuanza kutafuta bao la kusawazisha na jitihada zao zikazaa matunda kwani dakika ya 54 tu mshambuliaji Jarrof Bowen alifanikiwa kuisawazishia West Ham bao na ubao kusomeka 2-2.ArsenalMpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yaliendelea kubaki ya mabao mawili kwa mawili na Arsenal kudondosha alama katika michezo miwili mfululizo baada ya kufanya hivo dhidi ya Liverpool wikiendi iliyomalizika, Klabu hiyo inaendelea kusalia kileleni kwa alama nne dhidi ya Man City lakini vijana wa Pep Guardiola wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.