Klabu ya Arsenal na Liverpool wametoka sare katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliozikutanisha timu hizo na kila timu kufanikiwa kuondoka na alama moja katoka dimba la Anfield.
Klabu ya Arsenal ambao ndio vinara wa ligi kuu ya Uingereza walianza mchezo huo vizuri baada ya kupata mabao mawili ya haraka kupitia kwa Gabriel Martinelli na Gabriel Jesus kabla ya Mohamed kuipatia Liverpool bao moja kabla ya mchezo huo kwenda mapumziko na mchezo kufanikiwa kwenda mapumziko Washika mitutu wakiwa mbele kwa mabao mawili.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana kwa klabu ya Liverpool kuonekana kama wanahitaji kuasawazisha bao ambalo wametanguliwa, Vijogoo hao wa Anfield kutokaana na mashambulizi ambayo walikua wanafanya walifanikiwa kupata penati dakika ya 54 na Mohamed Salah kukosa mkwaju huo.
Klabu ya Arsenal walionekana kukaa nyuma kipindi kirefu huku wapinzani wao klabu ya Liverpool wakionekana kufanya mashambulizi mara kwa mara, Dakika ya 87 jitihada za Liverpool zilionekana kuzaaa matunda ambapo mshambuliaji Roberto Firmino alifanikiwa kuisawazishia Liverpool bao na mchezo kumalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.
Arsenal baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa leo dhidi ya Liverpool sasa wanafikisha jumla ya alama 73 na kuendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya alama sita lakini Man City wakiwa na mchezo mkononi, Huku Liverpool wao walifanikiwa kufikisha alama wakifikisha alama 44 lakini wakiendelea kusalia nafasi ya nane kwenye msima

