Crystal Palace Yaisambaratisha Leeds United

Klabu ya Crystal Palace imefanikiwa kuishangaza klabu ya Leeds United baada ya kuifunga kwa mabao matano kwa moja katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la Elland Road.

Crystal Palace wakiwa ugenini wamefanikiwa kuonesha ubora mkubwa katika mchezo wa leo dhidi ya Leeds United  na kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono kabisa, Leeds United walifanikiwa kupata bao la mapema mbele ya Palace lakini vijana wa Hodgson wakaweza kurejea na kushinda mchezo.Crystal palacePatrik Bamford alifanikiwa kuitanguliza klabu ya Leeds United kupata bao la kuongoza dakika ya 21 ya mchezo kabla ya Marc Guehi kusawazisha dakika ya 45 ya mchezo na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya bao moja kwa moja.

Kipindi cha pili Crystal Palace walikuja kwa kasi zaidi na kufanikiwa kupata goli la pili kupitia kwa Jordan Ayew dakika ya 53 kabla ya Eberechi Eze na Odsonne Oduard kuongeza bao la tatu na la nne na Jordan Ayew kupigilia msumari bao la tano kukamlisha karamu ya mabao katika mchezo wa leo.Crystal palaceCrystal Palace wamefanikiwa kushinda michezo miwili mfululizo ya ligi kuu ya Uingereza na michezo yote wamekua wakitoka nyuma na kufanikiwa kushinda mchezo, Hii inaonesha baada ya kocha Roy Hodgson kupewa timu ameleta mabadiliko makubwa kwa timu mpaka sasa wakikwea hadi nafasi ya 12 kwa alama zao 33.

Acha ujumbe