Varane Kurejea Kabla ya Msimu Kumalizika

Beki wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ufaransa Raphael Varane inaelezwa atarejea kabla ya msimu kumalizika kama ambavyo ilitarajiwa mwanzo kukaa nje msimu mzima.

Varane alipata majeraha katika mchezo wa robo fainali kombe la Europa uliopigwa katika dimba la Old Trafford na taarifa za awali zilieleza kua beki huyo atakosekana kwa msimu uliobakia, Lakini taarifa za ndani kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza mchezaji atarejea uwanjani kabla ya msimu kumalizika.VaraneBeki huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua na msimu mzuri ndani ya kikosi cha Manchester United tangu amejiunga na klabu hiyo kutoka Real Madrid mwaka 2021 akitengeneza safu nzuri ya ulinzi na beki Lisandro Martinez, Lakini majeraha yamekua sehemu ya jinamizi kwa beki huyo.

Beki Varane anaweza kurejea kabla ya msimu kumalizika kama ambavyo vyanzo vya ndani vya klabu hiyo vinaeleza, Lakini hataweza kucheza pamoja na beki mwenzake wa kimataifa wa Argentina Lisandro Martinez ambao wamekua wana ushirikiano mzuri kutokana na majeraha yanayomkabili na kua nje mpaka msimu ujao.VaraneKurejea kwa Varane inaweza kua taarifa nzuri sana kwa kocha wa Manchester United Erik Ten Hag pamoja na mashabiki wa klabu hiyo kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha beki huyo, Lakini pia kocha wa klabu hiyo ataweza kumtumia beki wake Luke Shaw kwenye eneo lake la beki wa kushoto kwani kwasasa anamtumia kama beki wa katikati.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.