Varane Kastaafu Timu ya Taifa ya Ufaransa

Aliyekua beki wa timu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane ametangaza kustaafu timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kuitumikia kwa muda nrefu na kwa mafanikio makubwa.

Beki Varane ameanza kuitwa timu ya taifa ya Ufaransa kwa mara ya kwanza mwaka 2012 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uruguay lakini hakutumika, Huku akianza kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2013 katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Goergia.VaraneBeki huyo anaondoka kwenye timu ya taifa ya Ufaransa akiwa miongoni mwa mabeki ambao wamecheza michezo mingi kwenye timu ya taifa ya Ufaransa akicheza michezo 90, Huku akiwa na mafanikio makubwa kwenye timu hiyo.

Raphael Varane akiwa amecheza michezo 90 kwenye timu ya taifa ya Ufaransa pia amefanikiwa kucheza fainali mbili za kombe la dunia huku akishinda fainali moja mwaka 2018, Vilevile amefanikiwa kushinda taji la michuano ya Uefa Nations League mwaka 2021VaraneRaphael Varane ataendelea kuitumikia klabu yake ya Manchester Unitedbaada ya kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa, Beki huyo pia kwa kipindi chote ambacho amekua katika timu ya taifa ya Ufaransa chini ya kocha Didier Deschamps alikua moja wachezaji muhimu ndani ya timu hiyo.

 

Acha ujumbe