Bellingham Kutua Madrid ni Suala la Muda

Kiungo wa kimataifa wa Uingereza anayekipa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Jude Bellingham inaelezwa yuko kwenye hatua za mwisho kumalizana na klabu ya Real Madrid ili kujiunga na mabingwa hao wa ulaya.

Vyanzo mbalimbali vya kuaminika kutoka nchini Hispania vinaeleza kua klabu ya Real Madrid imeshamalizana na kiungo Bellingham kwenye maslahi binafsi na sasa wanapanga mkutano wa mwisho na klabu ya Borussia Dortmund katika kuhakikisha dili hilo linamalzika kabla ya msimu huu kumalizika.BellinghamKiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua kwenye misimu miwili bora sana ndani ya klabu ya Borussia Dortmund na kuzivutia timu kubwa mbalimbali kutoka barani ulaya, Lakini ni Real Madrid ambao wanaelezwa wapo mwishoni kabisa kunasa saini yake.

Klabu ya Liverpool, Man United na Man City ni miongoni mwa vilabu vikubwa ambavyo vimekua vikihusishwa na saini ya Bellingham, Lakini kiungo huyo ameamua kujiunga na mabingwa wa ulaya klabu ya Real Madrid ikielezwa imekua ndoto yake ya muda mrefu kukipiga ndani ya timu hiyo.BellinghamReal Madrid wapo kwenye mkakati wa kutafuta mbadala wa viungo wake mahiri waliokipiga kwa mafanikio kwenye timu hiyo Luca Modric na Toni Kroos, Hivo Bellingham ni miongoni mwa viungo ambao wanakuja kwajili ya kuziba mapengo ya viungo hao mafundi tena kwa muda mrefu kwani kiungo huyo ndo kwanza ana umri wa miaka 19.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.