Manchester United Yamfukuzia Lautaro Martinez

Klabu ya Manchester United inataarifiwa inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayekipiga klabu ya Inter Milan ya nchini Italia Lautaro Martinez ili waweze kumsajili katika dirisha lijalo.

Lautaro Martinez amekua akionesha ubora mkubwa ndani ya klabu ya Inter Milan kwa muda mrefu sasa, Huku klabu ya Manchester United wao wakiwa wanatafuta mshambuliaji mwenye ubora mkubwa ili kuboresha safu yao ya ushambuliaji ambayo inaonekana kutokua na ubora mkubwa.manchester UnitedMan United wamekua wakitafuta mshambuliaji wa kiwango cha dunia kwa muda mrefu na wanahusishwa na washambuliaji kadhaa kama Harry Kane kutoka klabu ya Tottenham, Lakini inaelezwa hofu yao kubwa ni huenda wasiweze kumpata mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kutokana na ugumu wa bosi wa klabu hiyo Daniel Levy ndio sababu wamemgeukia Lautaro Martinez.

Manchester United chini ya kocha Erik Ten Hag wanataka kutengeneza timu yenye ushindani mkubwa na kuirudisha timu hiyo kwenye ubora wake, Hivo kitu kitakachoweza kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora ni pamoja na kufanya usajili wenye ubora.manchester UnitedLautaro Martinez mbali na Manchester United ameshahushwa na vilabu tofauti tofauti vikubwa duniani na mashetani hao wekundu nao wameonekana kuingia kwenye mbio hizo, Huku mshambuliaji inaelezwa aina yake ya uchezaji inamvutia zaidi kocha wa timu hiyo kwani ni aina ya washambuliaji anaowapenda.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.