Joao Felix Kurejea Atletico

Winga Joao Felix raia wa kimataifa wa Ureno ambaye alikua akiitumikia klabu ya Chelsea kwa mkopo akitokea klabu ya Atletico Madrid kutoka nchini Hispania imeelezwa atarejea kwenye klabu yake hiyo na hatabaki ndani ya Chelsea.

Taarifa kutoka ndani ya Chelsea zinaeleza kua kocha mpya wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino hamuoni Joao Felix kwenye mipango yake ya kuisuka timu hiyo kwa msimu ujao, Hivo ni wazi mchezaji huyo atarejea kwenye klabu yake mama baada ya mkopo wake kumalizika.joao felixJoao Felix alisaini mkataba mpya kabla ya kujiunga na Chelsea kwa mkopo kwenye dirisha dogo, Lakini klabu hiyo ilikua tayari kulipa kiasi cha pesa lakini kocha Pochettino ndio imeelezwa kua ndio ameamua kuruhusu mchezaji huyo aondoke kwakua haoni kama yupo kwenye mipango yake.

Rais wa klabu ya Atletico Madrid amethibitisha nae kua winga huyo wa kimataifa wa Ureno anarejea ndani ya klabu hiyo baada ya kocha wa klabu ya Chelsea kutokumuweka kwenye mipango yake, Hivo winga huyo ambaye hajakua na kipindi kizuri sana ndani ya Chelsea atarejea ndani ya viunga vya Wanda Metropolitano.joao felixJoao Felix licha ya kurejea ndani ya klabu ya Atletico Madrid lakini bado kuna vilabu mbalimbali vinamfatilia mchezaji huyo ili kupata huduma yake, Manchester United wanaelezwa ni miongoni mwa timu ambazo zinafukuzia huduma ya mchezaji huyo kwa karibu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.