Taarifa zinaeleza kua klabu ya Manchester United ipo kwenye mpango wa kuachana na mpango wa kumsajili golikipa wa klabu ya Inter Milan Andre ya Onana kwajili ya kiwango cha pesa.
Kiasi cha Euro milioni 55 ambacho klabu ya Inter Milan wameweka kwa golikipa huyo Manchester United wameona ni kiwango kikubwa kwa klabu hiyo kwani bajeti ya klabu hiyo katika majira haya ya joto sio kubwa kwa kiwango cha kuweza kutoa hela hiyo.
Taarifa zinaeleza kua Man United wanamfukuzia golikipa wa klabu ya Feyernoord ya ligi kuu ya Uholanzi Jim Bijlow ambaye wanaona kama bei yake itakua sio kubwa ukilinganisha na Andre Onana ambaye ni kiasi kikubwa cha pesa.
Bajeti ya Manchester United kwenye dirisha la usajili majira haya ya joto ni paundi milioni 100 ambapo mpaka sasa imeshatumika kiasi cha paundi milioni 55 kwa Mason Mount, Hivo klabu hiyo wanataka kufanya usajili wa kiwango kidogo cha pesa ili kuendana na bajeti hiyo.
Manchester United mpaka sasa wanategemea zaidi kuuza wachezaji ambao wapo klabuni hapo ili waweze kupata kiasi kingine cha pesa ambacho kitawasaidia kufanya usajili sokoni, Kwani kiasi cha paundi milioni 100 kwa klabu hiyo kinaonekana ni kiwango kidogo kuweza kutimiza mahitaji ya timu hiyo.

