West Ham Wamnyatia Ward Prowse

Klabu ya West Ham United mabingwa wa kombe la Uefa Conference League wanaripotiwa kumfukuzia kiungo wa klabu ya Southampton James Ward Prowse.

Kocha wa West Ham David Moyes inaelezwa kua ndo yupo mstari wa mbele kuhitaji huduma ya James Ward Prowse ambaye klabu yake ya Southampton imeshuka daraja hivo inaonekana kama kutakua na uwepesi fulani kumpata kiungo huyo.west hamKlabu ya Southampton yenyewe imedai inahitaji kiasi cha Puandi milioni 40 ili kumuachia mchezaji huyo, Hivo wapiga nyundo hao wanahitajika kufika bei ya waliyowekea kwa kiungo huyo ambapo amekua akifanya vizuri ndani ya klabu hiyo.

West Ham wanahitaji kuboresha timu yao kuelekea msimu ujao ambapo wanahitaji kuendelea kufanya vizuri kwenye michuano tofauti tofauti ambayo watakua wanashiriki ambapo wamekua mabingwa msimu uliopita wa michuano ya ulaya.west hamKlabu ya West Ham chini ya David Moyes wanahitaji kiungo mwingine ndani ya timu yao baada ya kuondokewa na nahodha wao Declan Rice ambaye amejiunga na klabu ya Arsenal hivo James Ward Prowse ameonekana chaguo zuri kwenye eneo la kiungo kwenda kuziba nafasi hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.