Manchester United Kutuma Ofa Rasmi kwa Hojland

Klabu ya Manchester United inatarajia kutuma ofa rasmi kwa klabu ya soka ya Atalanta kwajili ya kumnasa mshambuliaji wa klabu hiyo Rasmus Hojland raia wa kimataifa wa Denmark.

Manchester United baada ya kumaliza usajili wa golikipa Andre Onana sasa wamegeukia kwa mshambuliaji ambalo limekua tatizo lao la muda mrefu sasa, Huku Rasmus Hojland akiwa ndio kipaumbele chao zaidi baada ya kuachana na mpango wa kumnasa Harry Kane.Manchester UnitedMan United walikua na machaguo kadhaa ya washambuliaji mezani lakini jina pekee ambalo limebaki na linapewa nafasi na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag na klabu ya Atalanta wanaripotiwa kuhitaji kiasi cha euro milioni 65 mpaka 70.

Manchester United wameonekana wako makini kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao kutokana na namna wanafanya sajili zao kuelekea msimu ujao, Kwani mpaka sasa wameshafanya sajili mbili ambazo zinaonekana ni muhimu kwao.Manchester UnitedKocha wa klabu ya Manchester United inaelezwa ndio anapambana sana dili za wachezaji ambao anawataka zikamilike mapema, Kwani anahitaji kupata wachezaji hao mapema ili awepo nao katika maandalizi kwajili ya msimu mpya.

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.