Klabu ya Chelsea inaripotiwa kukaribia muafaka na klabu ya Brighton kwajili ya kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ecuador Moises Caicedo.
Chelsea ambao walikataliwa dau lao juu ya kiungo huyo wiki kadhaa zilizopita ambalo lilikua paundi milioni 60 lakini wababe hao kutoka jijini London wanaripotiwa kutoa kiasi cha zaidi ya paundi milioni 70 na nyongeza kidogo ambayo watailipa baadae.Kiungo Moises Caicedo yeye kwa upande wake anahitaji kutimkia klabu hiyo kutoka jijini London, Lakini kinachosubiriwa ni makubaliano tu baina ya vilabu hivo viwili ndio vitahalalisha kiungo huyo kucheza katika viunga vya Stamford Bridge.
Chelsea chini ya kocha Mauricio Pochettino wanahitaji kubadili safu ya kiungo ya klabu hiyo na kutengeneza safu nyingine, Huku Caicedo akiwa moja ya wachezaji ambao wanahitajika kuja kuunda safu mpya ya kiungo ya klabu hiyo kuelekea msimu ujao.Moises Caicedo anataka kuitumikia Chelsea hili liko wazi licha ya kiungo huyo kusaini mkataba mpya wa kuitumikia Brighton mwezi Januari, Kutokana na hali hiyo inawasukuma zaidi matajiri hao kutoka jijini London kwani mchezaji mwenyewe ameonesha nia ya kujiunga nao.