Kocha Mkuu Wa Yanga Sc Miguel Gamondi amesema kuwa anajua ukubwa wa siku ya Mwananchi na anaelewa ukubwa wa mechi yao na Kaizer Chiefs.
Akizungumzamara ya kwanza mbele ya waandishi wa habari Gamondi alisema: “Kesho ni siku kubwa kwa Mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania Klabu hii kubwa yenye historia kubwa.
“Kwenye upande wa timu bado tuko kwenye maandalizi, na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs tutautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yetu kwa msimu ujao.”

