Kocha wa klabu ya Manchester Erik Ten Hag amesema suala la winga wa klabu hiyo ambaye amekua nje ya uwanja muda mrefu Mason Greenwood litaamuliwa na klabu.
Mason Greenwood amekua nje ya uwanja kwa muda wa mwaka mmoja na nusu sasa kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia, Lakini hivi karibuni aliachiwa huru baada ya kutopatikana na hatia jambo ambalo limefanya watu kufikiria anaweza kurudi ndani ya timu hiyo.Wakati akizungumza na wanahabari leo kuelekea mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Arsenal kesho kocha Erik Ten Hag amesema kua kuhusu jambo la Greenwood maamuzi yake yanatgemeana na klabu itaamua nini, Kocha huyo alishasema anatamani kua na mchezaji kama Greenwood miezi kadhaa nyuma lakini klabu ndio itaamua zaidi.
Klabu ya Manchester United ndio inasubiriwa kuamua kama itaendelea kubaki na mchezaji huyo ambaye mpaka sasa hajajiunga na wachezaji wenzake kambini, Huku sababu kubwa ikiwa ni maamuzi kutoka klabuni yanasubiriwa zaidi.Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kocha Ten Hag anatamani kua na Greenwood kwenye kikosi chake kutokana na ubora ambao mchezaji huyo alikua anaonesha kabla ya kua nje ya uwanja lakini klabu hiyo inataka kumtoa kwa mkopo kwanza nje ya Uingereza.