Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amesema kuondoka kwa winga wa kimataifa wa Ufaransa Klabuni hapo Ousmane Dembele kutawadhoofisha.
Xavi wakati akiongea na wanahabari kuzungumzia masulala mabalimbali ya klabu hiyo alisema anafurahishwa na mawinga waliopo ndani ya klabu hiyo, Lakini kuondoka kwa Dembele kuna namna kutacha pengo kwenye timu hiyo.
Winga Ousmane Dembele anatarajia kutimka klabuni hapo na kujiunga na mabingwa wa Ufaransa klabu ya PSG ambapo mpaka sasa wameshamalizana na yamebaki mambo machache kuweza kukamilisha dili hilo.
Kocha huyo na kiungo wa zamani wa klabu hiyo aliongeza pia kwa kusema alimuuliza Dembele ni sababu gani iliyomfanya akaichagua PSG mbele Barca na alichomjibu ni sababu binafsi ndio zimepelekea kutimka.
Kocha Xavi amekua akimuhitaji Dembele aendelee kubaki ndani ya klabu hiyo na hata mara kadhaa alipokua akihojiwa alikua anaeleza wazi kua winga huyo wa kimataifa wa Ufaransa ni mchezaji muhimu ndani ya timu hiyo na angehitaji kua nae kikosini.

