Beki mpya wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Uholanzi Jurrien Timber amepata majeraha ambayo yatapelekea kufanyiwa upasuaji siku chache zijazo.
Beki Jurrien Timber alipata majeraha katika mchezo wake wa kwanza tu alioichezea klabu ya Arsenal katika ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Nottingham Forest ambapo hakufanikiwa kumaliza mchezo huo na kutolewa nje.
Taarifa rasmi kutoka klabu ya Arsenal inaeleza kua beki huyo anatarajia kufanyiwa upasuaji kutokana na majeraha ambayo ameyapata katika mchezo wa juzi ambapo mpaka sasa taarifa za kua atakaa nje kwa muda gani hazijafahamika.
Beki huyo wa zamani wa klabu ya Ajax anatarajiwa kukaa nje kwa muda kidogo kutokana na kufanyiwa upasuaji, kwani kikawaida mchezaji alifanyiwa upasuaji hua wanakaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kidogo.
Klabu ya Arsenal imepata mapigo mawili ndani ya klabu hiyo kwani wiki kadhaa zilizopita mshambuliaji wa klabu hiyo Gabriel Jesus nae alipata majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa muda mrefu na sasa Jurrien Timber nae amepata majeraha ya muda mrefu.

