Jurrien Timber beki wa kimataifa wa Uholanzi aanayecheza klabu ya Ajax Amsterdam ameweka wazi juu ya yaliokua yanasemwa juu yake kuhusu kwenda Manchster United.
Ikumbukwe wakati kocha mpya wa Manchester United anafika klabuni hapo chaguo la kwanza kwenye nafasi ya ulinzi ilikua ni beki huyo aliekua akimfundisha katika klabu ya Ajax lakini hakufanikiwa kukamilisha dili hilo.
Taarifa nyingi zilielezwa kua alikatazwa na kocha wa timu yake ya taifa Luis Van Gaal kwenda kwenye klabu hiyo na kumtahadharisha kua akikosa nafasi ya kucheza hatapata nafasi kwenye timu amabayo inajiandaa kucheza michuano ya kombe la dunia mwishoni mwa mwaka huu.
Iliaminika hivo kwakua kocha huyo ambaye aliwahi pia kuifundisha Manchester United alinukuliwa akimsihi muholanzi mwenzake Eric ten Hag asijiunge na mashetani hao wekundu kwani timu hiyo ipo kibiashara zaidi kuliko kuwekeza kwenye mpira.
Jurrien ameeleza kua ni Van Gaal aliemueleza kua anaweza kwenda Manchester United na kupata dakika za kucheza hivo habari zilizokua zinaendelea kua kocha huyo ndo alimuambia asijiunge na klabu ya Manchester United sio taarifa za kweli.

