Greenwood Akipiga Getafe Ikishinda

Winga wa Manchester United Mason Greenwood ambaye yupo kwa mkopo klabu ya Getafe ya nchini Hispania amefanikiwa kucheza mchezo wake wa kwanza huku klabu yake ikipata matokeo ya ushindi.

Greenwood amefanikiwa kucheza kwa mara ya kwanza baada ya kukaa nje ya uwanja kwa kwa muda mrefu takribani mwaka mmoja na nusu, Huku akiwa sehemu ya kikosi kilichopata matokeo ya ushindi dhidi ya Osasuna.greenwoodWinga huyo raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye aliingia mnao dakika ya 77 ya mchezo ambapo matokeo yalikua mabao mawili kwa mawili mpaka dakika hiyo huku winga huyo akifanikiwa kusababisha kona iliyozaa bao la tatu.

Klabu ya Getafe inafanikiwa kushinda mchezo wake wa pili katika ligi kuu ya Hispania na kufikisha alama 7, Huku pia winga huyo wa zamani wa Man United akicheza mchezo wake wa kwanza leo wa kiushindani tangu akae nje ya uwanja kwa muda mrefu.greenwoodWinga Mason Greenwood ameonekana bado ana umahiri na ubora licha ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na ubora ambao ameuonesha leo japo sio asilimia 100 ya ubora wake unaojulikana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.