Klabu ya Chelsea mambo bado yanaendelea kuwaendea upande kwani leo tena wameshindwa kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya AFC Bournamouth.

Chelsea imelazimishwa sare leo ya bila kufungana na klabu ya AFC Bournamouth katika mchezo wao wa tano wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu, Huku wakishindwa kupata matokeo katika michezo miwili mfululizo.chelseaMatajiri hao kutoka jijini London bado wanaendelea kupata tabu katika kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi kwenye michezo yao licha ya kufanya usajili mkubwa na wa gharama kubwa klabuni hapo.

Vijana wa Mauricio Pochettino leo waliendelea na utaratibu wa kumiliki mchezo kwa kiwango kikubwa, Lakini matokeo ya ushindi ndio yameendelea kua kitendawili kwa klabu hiyo.chelseaChelsea sasa wamecheza michezo mitano ya ligi kuu ya Uingereza huku wakifanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee dhidi ya Luton Town, Huku wakipoteza michezo miwili na kutoa sare michezo miwili wakijikusanyia jumla ya alama tano.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa