Havertz Aanzia Nje kwa mara ya Kwanza

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Kai Havertz anayekipiga klabu ya Arsenal kwasasa ameanzia nje kwa mara ya kwanza ndani ya kikosi cha Arsenal kwa mara ya kwanza msimu huu.

Mshambuliaji Kai Havertz hajafanikiwa kuanza vizuri ndani ya klabu ya Arsenal ambayo amejiunga nayo katika dirisha kubwa lililopita na mashabiki wa klabu hiyo wakitaka aanzie nje na hatimae leo anaanzia nje dhidi ya Everton.havertzKocha Mikel Arteta ni kama amesikia kelele za mashabiki wa klabu hiyo ambazo walikua wanapiga kelele juu ya mchezaji huyo wakiamini hakua anastahili kuanza katika michezo ya klabu hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri katika michezo ya awali.

Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa wachezaji walisajiliwa kwa gharama ndani ya klabu ya Arsenal msimu huu, Hivo kushindwa kuonesha kiwango bora katika michezo ya timu hiyo ni jambo ambalo limekua likiwakwaza mashabiki wa klabu hiyo.havertzKiungo Fabio Viera ndio anaonekana kuingia kuchukua nafasi ya Kai Havertz katika mchezo wa leo dhidi ya Everton, Huku kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno akiwa moja ya wachezaji ambao walikua wanapigiwa chapuo kuanza kwani kila alikua akitokea nje anaonesha uwezo.

Acha ujumbe