Pochettino: Mudryk Anahitaji Muda

Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino amesema kua winga wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ukraine Mykhaylo Mudryk bado anahitaji muda wa kuendelea kujifunza na kuendana na mazingira.

Pochettino anasema winga huyo anaendelea kuboresha uwezo wake na mpaka sasa anaonesha amejiboresha kwa kiwango fulani, Hivo anahitaji muda zaidi wa kuendelea kuonesha ubora mkubwa zaidi.pochettinoWinga huyo amekua nyuma ya matarajio ya klabu hiyo tangu aliposajiliwa mwaka huu mwezi Januari kwa gharama kubwa ya usajili jambo ambalo linaendelea kumpa presha winga huyo mwenye umri mdogo.

Kocha Pochettino amesema kua winga Mudryk anahitaji kuuelewa mchezo vizuri zaidi ili kupata muunganiko zaidi na timu, Huku akiongeza wanahitaji kumpa muda zaidi ili aboreshe ubora wake kwa kiwango cha juu zaidi.pochettinoWinga Mudryk alikua na kiwango bora sana akiwa na klabu ya Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine, Lakini mambo yamebadilika tangu amejiunga na Chelsea huku kocha wake akiamini mchezaji huyo atarejesha makali yake anahitaji muda tu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.