Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ameeleza kwanini golikipa David Raya ameanza katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya Uingereza na golikipa namba moja wa klabu hiyo Aaron Ramsdale kukaa benchi.
Kocha Arteta amesema kua sababu ya kuanza kwa David Raya ni kuhakikisha wanafanya mzunguko katika kikosi hicho, Kwani wanahitaji ubora katika kila nafasi uwanjani.David Raya raia wa kimataifa wa Hispania ambaye amekua kwenye kiwango bora akiwa na klabu ya Brentford, Amefanikiwa kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa katika milingoti ya klabu ya Arsenal dhidi ya Everton leo.
Kocha Mikel Arteta ameeleza kitu ambacho walikipanga ni kuhakikisha wanapata mchezaji mwenye ubora katika kila nafasi uwanjani na ndio kitu ambacho kinafanyika sasa ndani ya timu hiyo.Baada ya kauli ya kocha wa klabu hiyo na kiungo wa zamani wa klabu hiyo ni wazi inaonesha kua Arsenal wameboresha kikosi chao kwa wachezaji bora, Kwani leo amepumzishwa golikipa namba moja anacheza namba mbili mwenye ubora.