Arsenal Yachukua Tatu Muhimu Goodison Park

Klabu ya Arsenal imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kufanikiwa kupata alama tatu muhimu katika dimba la Goodison Park katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Everton.

Arsenal wamefanikiwa kutoka na alama tatu wakiwa ugenini katika mchezo mgumu dhidi ya Everton leo ambapo wamefanikiwa kushinda kwa bao moja kwa bila bao pekee lililofungwa na Leandro Trossard.arsenalVijana wa Mikel Arteta kama kawaida walimiliki mpira kwa kiwango kikubwa katika mchezo wa leo na walionekana wanaitaka mechi kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo, Lakini Everton nao hawakua na unyonge kwani walizuia kwa ufanisi mkubwa.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa klabu hizo kumalizika kwa sare ya bila kufungana licha ya Arsenal kufunga bao kupitia kwa Gabriel Martinelli, Lakini bao hilo lilikataliwa kutokana na mchezaji huyo kuotea kwa msaada wa marudio ya Video VAR.arsenalMchezaji Leandro Trossard ndio aliyeifanya mechi kua tofauti badala ya kuisha kwa sare ya bila kufungana kwani ndio aliyefunga bao pekee la mchezo huo baada ya kuchukua nafasi ya Gabrielli Martinelli aliyepata majeraha kipindi cha kwanza.

Washika mitutu hao kutoka jiji la London baada ya ushindi wa leo dhidi ya Everton sasa wanafikisha jumla ya alama 13 baada ya kucheza michezo mitano, Huku wakiendelea kukaa kwenye kundi la timu ambazo hazijapoteza mchezo mpaka sasa wakiwa wameshinda michezo minne na kusuluhu mchezo mmoja.

Acha ujumbe