Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kulingana na ratiba sio rafiki wachezaji wake Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho kuwa muda wote hawawezi kucheza kwa kiwango bora zaidi.

Amesema anaridhishwa na kiwango cha wachezaji wake inawezekana kuna nyakati mambo hajaenda sawa lakini haangalii mchezaji mmoja mmoja huwa anaangalia zaidi matokeo ya timu.
“Mchezaji kuwa na siku mbaya kazini ni kawaida duniani kote hata wachezaji waku Ulaya mfano Kylian Mbape, hata hivyo naridhika na mwenendo wa wachezaji wangu wote.
Sina wasiwasi kabisa na timu yangu, sijui hayo yanatoka wapi kuwa unajua mpira huwezi kuwa na mashaka na Yanga nafikiri wale wanajiuluza uluza maswali watapata majibu, muda utaongea,” amesema Gamondi.


