GAMONDI AWAKINGIA KIFUA AUCHO NA AZIZI KI

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kulingana na ratiba sio rafiki wachezaji wake Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho kuwa muda wote hawawezi kucheza kwa kiwango bora zaidi.

GAMONDI AWAKINGIA KIFUA AUCHO NA AZIZI KI

Amesema anaridhishwa na kiwango cha wachezaji wake inawezekana kuna nyakati mambo hajaenda sawa lakini haangalii mchezaji mmoja mmoja huwa anaangalia zaidi matokeo ya timu.

“Mchezaji kuwa na siku mbaya kazini ni kawaida duniani kote hata wachezaji waku Ulaya mfano Kylian Mbape, hata hivyo naridhika na mwenendo wa wachezaji wangu wote.

Sina wasiwasi kabisa na timu yangu, sijui hayo yanatoka wapi kuwa unajua mpira huwezi kuwa na mashaka na Yanga nafikiri wale wanajiuluza uluza maswali watapata majibu, muda utaongea,” amesema Gamondi.

GAMONDI AWAKINGIA KIFUA AUCHO NA AZIZI KI

Kuhusu mchezo wa leo dhidi ya Pamban jiji, amesema ratiba sio rafiki sana ya wachezaji kujiandaa na kuwa na utimamu wa kimwili, wapo tayari kwa mchezo huo. Anajua wanakutana na mchezo mgumu .

Ameeleza kimsingi hawapati shida sana kwa kuwa wamejipanga kiakili na kimwili wapo imara , Pamba jiji hawajashinda mchezo wowote, wamepanda daraja labda wanapata radha sahihi ya kucheza ligi .

“Nafahamu uimara wao wameruhusu mabao matano katika mechi sita, wamefunga mawili tumefanya utafiti wetu na timu inayokaa sana nyuma,” amesema Kocha huyo wa Yanga.

Acha ujumbe