MORINYO WA YANGA AANDIKA REKODI KWA SIMBA QUEENS

Timu ya Yanga Princess imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya Ngao ya Jamii kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 na watani, Simba Queens jioni ya Jana kwenye Uwanja Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.

MORINYO WA YANGA AANDIKA REKODI KWA SIMBA QUEENS

Yanga Princess walitangulia kwa bao la dakika ya kwanza tu la kupitia kwa Kiungo Mpya wa Timu Hiyo Agness Palangyo, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya, Jentrix Shikangwa Milimu kuisawazishia Simba Queens dakika ya 88.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

MORINYO WA YANGA AANDIKA REKODI KWA SIMBA QUEENS

Ushindi huo unamfanya Kocha Mkuu wa Timu Hiyo na Mwenye mbwembwe nyingi Edna Lema (Morinyo) kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu ya kuwa kocha wa kwanza wa Yanga Princess kuwafunga Simba Queens mara mbili na kuwa kocha wa kwanza kuipeleka Timu Hiyo Fainali ya Ngao ya Jamii.

Yanga Princess’s watacheza fainali ya JKT Queens na Simba Queeens watacheza kusaka mshindi wa tatu na Ceasiaa Queens kesho kutwa tarehe 5.

Acha ujumbe