Klabu ya Yanga imeanza mikakati kabambe ya kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao wa jadi, Simba, unaotarajiwa kupigwa, Septemba 16, mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Arafat Haji, amesema kuwa mipango na mikakati ya mechi hiyo imeshaanza ambapo lengo ni kupata ushindi ili kuendelea kulihifadhi taji hilo. Alisema kuwa heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26, itaanza kuwekwa katika mchezo huo.




