Simba SC Yatangaza Rasmi Kikosi Kipya 2025/26

Ikiwa ni siku iliyosheheni shamrashamra na hisia za mashabiki wa soka, Simba SC imetangaza rasmi kikosi chake cha msimu wa 2025/2026 kupitia tamasha la Simba Day lililofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Hafla hiyo, ambayo imekuwa sehemu ya utamaduni wa klabu hiyo, iliwakutanisha maelfu ya mashabiki waliokuwa na kiu ya kuona sura mpya zitakazowakilisha wekundu wa Msimbazi msimu huu.

Simba SC Yatangaza Rasmi Kikosi Kipya Simba Day

Meneja wa Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally, aliongoza utambulisho wa wachezaji 30 walioteuliwa kuunda kikosi kipya, akisisitiza kuwa msimu huu Simba imejipanga kwa ubora wa hali ya juu. Miongoni mwa waliotambulishwa ni nyota chipukizi waliopandishwa kutoka kikosi cha vijana, akiwemo Bashir Kibaila, Hussein Mbegu, na Alexander Erasto. Wachezaji hao, wote wakiwa na umri wa miaka isiyozidi 20, wanatazamwa kama sehemu ya kizazi kipya chenye njaa ya mafanikio na uwezo wa kuleta mabadiliko uwanjani.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika muundo wa kikosi, Simba imeonyesha uwiano mzuri wa wachezaji katika kila idara. Safu ya ulinzi na kiungo imejumuisha wachezaji kumi kwa kila upande, ikionyesha mkakati wa kudhibiti mchezo na kuimarisha ngome. Washambuliaji sita wamechaguliwa kwa uwezo wao wa kutengeneza nafasi na kufunga mabao, huku langoni kukiwa na makipa wanne waliothibitisha ubora wao katika mechi za awali.

Simba SC Yatangaza Rasmi Kikosi Kipya Simba Day

Mbali na wachezaji, Simba SC pia imetangaza benchi lake la ufundi lenye wataalamu 13, likiongozwa na kocha mkuu kutoka Afrika Kusini, Fadlu Davids. Akizungumza mara baada ya kutambulishwa, Davids alitoa ujumbe wa matumaini kwa mashabiki wa klabu hiyo, akieleza kuwa msimu huu ni wa kuandika historia mpya. Alikumbusha kuwa msimu uliopita klabu ilikaribia kutwaa mataji, lakini safari ya mwaka huu inalenga mafanikio halisi. “Tunawaheshimu mashabiki wetu kwa sapoti yao ya dhati. Msimu huu ni wa ushindi,” alisema kwa kujiamini.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.