Klabu ya Fountain Gate kesho Jumapili, itafanya tamasha ndogo la kutambulisha wachezaji wake wapya watakaotumika msimu huu. Tamasha hilo lililopewa jina la Tanzanite Day, litafanyika kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, uliopo Wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Hatua hiyo inakuja baada ya timu hiyo kupewa ruhusa ya kusajili wachezaji wake wapya, ambao walikwama kuingia kwenye mfumo baada ya kufungiwa kusajili kutokana na madeni.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Mratibu wa Fountain Gate, Wendo Makau, alisema: “Tamasha hili ni dogo lakini lenye maana kubwa sana kwa watu wetu wa Babati, tunataka tukutane nao na wawaone wachezaji wao.”