Nahodha wa Senegal, Sadio Mane amesema kuwa aliamua kuwakataza wenzake kugomea mechi ya fainali ya AFCON 2025 dhidi ya Morocco jana kwa kuwa tukio hilo linaharibu taswira ya soka kwa ujumla katika dimba la Prince Moulay Abdallah.

Katika dakika za lala salama za mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Senegal, Pape Thiaw aliwaamuru wachezaji wake kutoka nje ya uwanja kufuatia uamuzi wa Refa Jean-Jacques Ndala kuamuru penalti kwenda langoni mwao baada ya Brahim Diaz kufanyiwa faulo na Malick Diouf katika dakika za mwisho mwisho zamchezo.
Hata hivyo nahodha wa Senegal Sadio Mane alionekana kutokubaliana na uamuzi wa kuondoka uwanjani ambapo alionekana akiwashawishi wenzake kuendelea na mchezo.
Akizungumzia mchezo huo, Mane anasema kuwa kwake ni bora wangepoteza mechi kuliko kugomea mchezo.
Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.


