Simba SC Yampa Kwaheri Steven Mukwala

Simba SC imefikia maamuzi magumu lakini ya kimkakati kwa kumruhusu aliyekuwa mshambuliaji wake, Steven Desse Mukwala, kuondoka rasmi na kujiunga na Klabu ya Al Nasser inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Libya. Hatua hii inaashiria mwisho wa safari ya Mukwala katika ardhi ya Tanzania baada ya kuitumikia Simba katika vipindi tofauti vya ushindani wa ndani na kimataifa.

Al Nasser wamemtambulisha Mukwala kama mchezaji wao mpya saa chache tu baada ya Simba SC kutoka sare dhidi ya Mtibwa Sugar, jambo linaloonyesha kuwa dili hilo lilikuwa tayari limekamilika mapema. Utambulisho huo umefanyika kwa kasi kubwa, ishara kwamba klabu ya Libya ilikuwa na mpango maalum wa kumwingiza mshambuliaji huyo mara moja kwenye mipango yao ya kikosi.

Simba Sc Yampa Kwaheri Steven Mukwala

Kuondoka kwa Mukwala hakujaja kwa bahati mbaya. Simba SC imekuwa ikipitia kipindi cha tathmini ya kikosi chake, ikilenga kuongeza ushindani, uwiano wa ubora na mahitaji ya kifedha. Kwa Mukwala, fursa ya kucheza Ligi Kuu ya Libya ni hatua mpya ya maendeleo ya taaluma yake, huku Simba ikipata nafasi ya kufanya maboresho zaidi katika safu ya ushambuliaji.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mukwala anakuwa mchezaji wa pili wa kimataifa kuondoka Simba SC katika dirisha dogo la usajili, baada ya Jean Charles Ahoua. Mabadiliko haya yanaonyesha wazi kuwa Simba ipo katika awamu ya mabadiliko, ikijenga upya kikosi chake kwa malengo ya muda mrefu, hasa katika mashindano ya ndani na yale ya Afrika.

Simba Sc Yampa Kwaheri Steven Mukwala

Kuondoka kwa wachezaji hawa wa kimataifa kunafungua milango ya nyota wapya kusajiliwa na wekundu hao wa msimbazi. Macho yanabaki msimbazi kuona ni sajili zipi mpya zitafanyika ndani ya kikosi hicho

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.