Simba SC Kuwakosa Gueye Na Kapombe Dhidi ya Stade Malien

Klabu ya Simba SC itamkosa winga wake, Libasse Gueye, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien utakaopigwa kesho, kufuatia adhabu ya kadi nyekundu. Gueye anatumikia adhabu hiyo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Petro de Luanda.

Katika mchezo huo, beki Shomari Kapombe alioneshwa kadi nyekundu wakati mpira ukiendelea, huku Gueye akitolewa nje baada ya filimbi ya mwisho kufuatia mabishano na mwamuzi wa mechi. Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mchezaji anayepata kadi nyekundu hukosa angalau mechi moja inayofuata katika mashindano husika.

Simba SC Kuwakosa Gueye Na Kapombe Dhidi ya Stade Malien

Kutokuwepo kwa Gueye kunatajwa kuwa pigo kwa Simba SC, hasa kutokana na mchango wake katika eneo la ushambuliaji. Winga huyo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi katika michuano ya kimataifa, akitoa ubunifu katika safu ya mbele. Benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Barker, linatarajiwa kufanya mabadiliko ya kikosi ili kuziba pengo hilo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa upande mwingine, Stade Malien wanatarajiwa kuingia uwanjani wakiwa na morali ya juu wakilenga kupata matokeo chanya ugenini. Klabu hiyo yenye makazi yake Bamako, Mali, ina uzoefu katika mashindano ya CAF na imekuwa ikiwasumbua wapinzani wake kiuchezaji na uimara wa safu ya ulinzi.

Simba SC Kuwakosa Gueye Na Kapombe Dhidi ya Stade Malien

Ingawa mchezo huu hauna faida kwa Simba SC kwenye michuano hii lakini ni mchezo muhimu kwa kikosi cha Stade Malien katika harakati za kusaka alama muhimu hatua ya makundi ili kumaliza nafasi ya kwanza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.